Yanga itakuja kivingine msimu ujao - Dk Nchemba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jul 2021
Yanga itakuja kivingine msimu ujao - Dk Nchemba

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini klabu ya Yanga Dk Mwigulu Nchemba amesema kwa michakato wanayoendelea nayo ndani ya klabu hiyo, msimu ujao utakuwa wa furaha kwa Wanachama na Mashabiki wa mabingwa hao wa kihistoria

Ligi Kuu msimu huu inakwenda kufikia tamati mwishoni mwa wiki hii huku klabu ya Simba ikiwa imetwaa ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo

Mh Nchemba ambaye pia ni Waziri wa fedha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema msimu ujao Yanga itakuwa na kikosi bora kitakachotikisa ligi ya ndani na michuano ya Kimataifa ambayo watashiriki baada ya kujihakikishia kumaliza nafasi tatu za juu VPL  huku pia wakiwa wametinga fainali ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)

Dk Nchemba amesema matunda ya Mabadiliko yanayoendelea ndani ya Yanga yataanza kuonekana msimu ujao

"Kwanza lazima ifahamike, hatukuwa na timu mbaya msimu huu ndio maana unaona tunaenda kushiriki mashindano ya CAF. Ukitaka kujua kwamba hicho kikosi ni imara, unaweza ukaangalia timu ambayo iliifunga Al Ahly ya Misri hapa, imepigwa goli dakika ya (11') na haikufurukuta kabisa kuweza kurudisha"

"Lakini kubwa ni haya Mabadiliko ambayo yanaendelea kufanyika, yatazidi kutuimarisha. tutakuwa na kikosi bora cha kuweza kufanya vizuri kwenye mashindano makubwa, Tutafanya usajili wakutisha kujenga kikosi chetu," alisema Dk Nchemba

Aidha kuelekea mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili Julai 25, Dk Nchemba amesema ni kawaida kwa Simba kutamba sana lakini baada ya dakika 90 wanakuwa 'wapole' hivyo ana imani Yanga itashinda mchezo huo

"Kusema wale jamaa wenzetu Simba hawaishagi maneno kwa hiyo huwa tunawaacha waseme wee, sie tukienda Kigoma tunawanyamazisha kwa kipigo"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’