Siku chache baada ya Uongozi wa Yanga kupaza sauti kwa manispaa juu ya miundo mbinu mibovu inayozunguka uwanja wa Kaunda, Mhandisi Makuu wa Manispaa ya Ilala,John Magori, leo amefika makao makuu ya Yanga kujionea hatua za mwanzo za ukarabati wa uwanja wa Kaunda.
Katika ziara hiyo fupi Mhandisi Magori alipata nafasi ya kuonyeshwa eneo zima la uwanja huo na kuelezwa changamoto kadhaa zilizopo katika hatua za uwekaji kifusi, kisha kutoa pongezi,ushauri na mapendekezo kadhaa
Magori ameomba kukutana na uongozi wa Yanga siku ya Jumanne na ameomba kupelekewa plani itayotumika katika ujenzi wa Uwanja.
Jana Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alitoa malalamiko kwa Manispaa ya Ilala juu ya mtaro wa maji machafu uliopita karibu na uwanja ambao unamwaga maji machafu uwanjani.

ADVERTISE HERE