Kama umepita maeneno ya Makao Makuu ya klabu ya Yanga Mtaa wa Twiga na Jangwani, bila shaka umeshuhudia Makandarasi wakiendelea na kazi ya kuboresha uwanja wa Kaunda
Uongozi wa Yanga umedhamiria kukamilisha maboresho ya uwanja huo haraka ili uanze kutumika
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amesema Wanachama na Mashabiki wa Yanga wakae tayari kwani kuna mambo mazuri watayashuhudia hivi karibuni katika uwanja huo wenye historia kubwa
Yanga kwa sasa imeweka kambi Mji wa Avic Town, Kigamboni wakati ikisubiri ujenzi wa Complex yake huko Kigamboni
Kama Uwanja wa Kaunda utakamilika, wanaweza kuutumia wakati ujenzi wa kule Kigamboni ukiendelea
Aidha Uwanja huo pia unaweza kutumiwa na timu ya Wanawake, Yanga Princess ambayo pengine inaweza kuweka kambi hapo Jangwani
Ukarabati wa vyumba 28 vya jengo la Makao Makuu unaendelea