Julai 25 kinapigwa tena mkoani Kigoma! Ni mchezo wa fainali ya kombe la FA kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Lake Tanganyika
Wakati Yanga ikiendelea na maandalizi ya mchezo huo, Mamlaka za usimamizi wa soka mkoani Kigoma, zinaendelea kuuweka uwanja huo sawa ili siku hiyo kusiwa na visingizio
Kazi kubwa imefanyika kubadili mandhari ya uwanja huo, bado wataalamu wanaendelea kuboresha zaidi
Tutafumua mshono - Injinia Hersi
Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Injinia Hersi Said amesema kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu
Hersi amesema Yanga imedhamiria kufumua 'mshono' ambao waliwashona Simba walipokutana uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mchezo wa ligi wiki iliyopita
"Sisi tunaendelea na maandalizi kila kitu kinakwenda vizuri. Nikuhakikishie, tunakwenda kufumua mshono tuliwashona wiki iliyopita," alitamba Injinia Hersi
Kabla ya mchezo huo, timu zote zitakuwa na michezo ya kukamilisha ratiba ya Ligi Kuu ambapo Yanga imesalia na michezo miwili dhidi ya Ihefu Fc na Dodoma Jiji

