Mapema leo, klabu ya Yanga iliingia makubaliano ya mkataba na Azam Media ya mashirikiano ya maudhui wenye thamani ya Shilingi bilioni 41 pamoja na VAT kwa kipindi cha miaka 10.
Makubaliano hayo yametiwa sahihi na Tido Mhando ambaye ni Afisa mtendaji mkuu wa Azam Media pamoja na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Dkt. Mshindo Msolla
Katika mwaka wake wa kwanza Yanga itavuna takribani Bilioni 2.4 ambayo ni sawa na kuvuna Tsh Milioni 200 kila mwezi
Yanga inaweza kuvuna zaidi ya Bilioni 3 kila mwaka kama itamaliza nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa ligi kuu
Wenyewe Wananchi wanasema fedha ambazo watakusanya kupitia makubaliano hayo zinaweza kununua klabu moja kubwa nchini na salio likabaki


ADVERTISE HERE