Wanachama wa Yanga Mwanza waja na mkakati wa kusajili wachezaji 10

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Dec 2017
Wanachama wa Yanga Mwanza waja na mkakati wa kusajili wachezaji 10
Wanachama wa matawi ya Yanga mkoani Mwanza wamekutana katika mkutano wao wa mwisho wa mwaka wenye lengo la kujadili mustakabali na mwenendo klabu yao katika msimu huu.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga wanachama hao kupitia kwa Mwenyekiti wa Matawi hayo, Salehe Akida wamedhamiria kufanya harambee katika matawi yote ya Mkoa wa mwanza ili kuhakikisha wanapata fedha za kuwawezesha kusajili wachezaji 10 katika msimu ujao kama nia na lengo la kuweza kua karibu na timu yao.

"Hakika tumedhamiria kufanya makubwa katika msimu ujao kwa kuweza kuyafanya matawi yetu ya wanachama wa Mwanza kuwa yakuigwa na kuwa mfano katika matawi yote Tanzania".

katika hatua nyingine wanachama hao wanechangishana fedha tasilimu shilingi laki tisa na elfu thelathini kwa lengo la kuwapa motisha wachezaji kuweza kujituma katika mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbao FC utaokaochezwa siku ya jumapili kwenye uwanja wa CCM kirumba mwanza majira ya saa kumi kamili jioni.

Akizungumza katika mkutano huo makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga Amewashukuru wanachama hao kwa umoja wao wanaouonesha katika kuinga mkono timu yao kwa kusafiri kwenda kuipa hamasa na kuwataka watulie ili waweze kuutetea ubingwa wao msimu huu.

"Yanga ni taasisi kubwa na inawanachama Tanzania Nzima wote nia yetu ni kuhakikisha yYnga inasonga mbele na asitokee mtu yeyote kutuvuruga na akitokea mtu huyo basi tumchukulie hatua mara moja ili kuiboresha yanga yetu"

Huu ni mkutano wao wa nne baada ya mikutano mitatu iliyofanyika mwaka huu katika Mkoa wa Mwanza ambao ni desturi yao kwajili ya kujulishana kinachoendelea katika kila matawi

Kwa hisani ya Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’