Baada ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Julai 18, kiungo mshambuliaji Deus Kaseke, atakuwa amemaliza mkataba wake na Yanga
Habari njema ni kuwa tayari mwamba huyu amehakikishiwa na uongozi wa Yanga kupata mkataba mwingine wa miaka miwili
Huu umekuwa msimu bora sana kwa Kaseke ambaye mwanzoni mwa msimu wapo waliohoji kiwango chake
Sasa ni mchezai aliyekomaa na kujihakikishia namba katika kikosi cha kocha Mohammed Nasreddine Nabi
Ameweka kambani mabao nane na kutoa pasi sita za usaidizi katika mashindano yote
Kaseke ndiye mchezaji mwandamizi zaidi katika kikosi cha sasa cha Yanga ukimtoa Haruna Niyonzima
ADVERTISE HERE