Shirikisho la soka nchini (TFF) limetoa leseni kwa wachezaji wapya waliosajiliwa katika usajili wa dirisha dogo lililofungwa Disemba 23, 2017.
TFF imeziruhusu timu zilizosajili wachezaji wakati huo kuanza kuwatumia tangu jana Disemba 29.
Afisa Habari Msaidizi wa TFF, Clifford Ndimbo amethibitisha kutolewa kwa leseni hapo jana Ijumaa.
Ndimbo alisema leseni hizo zilichelewa kutoka kutokana na TMS kusumbua, hivyo tayari wamezitaarifu klabu zote kuwa ni ruksa kuwatumia wachezaji wapya kuanzia mechi za jana Ijumaa.
Kwa maana hiyo Yanga sasa inaweza kuanza kuwatumia wachezaji wake wawili iliyowasajili beki Fiston Kayembe Kanku na mshambuliaji Yohana Mkomola.
Hii ni habari njema kwa Benchi la Ufundi la Yanga ambalo katika mchezo wa kesho litawakosa wachezaji wake muhimu kutokana na majeruhi na sababu nyinginezo.

ADVERTISE HERE