Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba mwishoni mwa wiki, nyota wa Yanga walipewa mapumziko ya siku tatu
Kesho Jumatano wanarejea kambini kujiandaa na mechi mbili za kumaliza msimu
Yanga imesalia na michezo miwili dhidi ya Ihefu Fc na Dodoma Jiji
Mchezo dhidi ya Ihefu utapigwa Julai 14 na Julai 18 watasafiri mkoani Dodoma kumaliza msimu dhidi ya Dodoma Jiji
Kimahesabu, Yanga bado iko kwenye mbio za ubingwa kwani pamoja na Simba kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa huo, bado wanahitaji kupata sio chini ya alama tatu
Aidha alama moja kutoka mechi zilizobaki inatosha kuihakikishia Yanga kumaliza nafasi mbili za juu
ADVERTISE HERE