Bonus watakayopata wachezaji haijawahi kutokea - Bumbuli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jul 2021
Bonus watakayopata wachezaji haijawahi kutokea - Bumbuli

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, wachezaji wa Yanga wanatarajiwa kukabidhiwa 'mkwanja' wa maana kwa kuwanyamazisha watani zao katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa juzi katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema baada ya mchezo dhidi ya Simba waliwapa wachezaji mapumziko ya siku tatu, watakaporejea watakabidhiwa bonus zao

"Wachezaji tuliwapa mapumziko ya siku tatu, watarejea kambini siku ya Jumatano.Kuhusu bonus iliyotengwa, haijawahi kutokea"

"Safari hii hatutapenda kutangaza, unajua wengine wanachukulia ushindi tunaopata unatokana na msukumo wa bonus. Lakini fahamu bonus watakayopata haijawahi kutokea," alisema Bumbuli

Katika hatua nyingine Bumbuli amesema bado wako katika mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Bumbuli amesisitiza kuwa bingwa wa ligi kuu atapatikana baada ya msimu kumalizika licha ya Simba kuonekana kuhitaji angalau alama tatu tu

"Bado tuna nafasi ya kuchukua ubingwa, na hata kama ikitokea tofauti huu ndio msimu wao wa mwisho kushinda. Tuna mechi na Ihefu tarehe 13 na baadae Dodoma Jiji tarehe 18, zote tunashinda. Ifikapo Julai 23 sisi tutakuwa mabingwa yaani kabla ya mchezo wa fainali ya FA tutakuwa tumetangazwa kuwa mabingwa," alisema Bumbuli katika mahojiano na Azam TV

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’