Baada ya kuachwa huru na Kamati ya Maadili kutoka kifungo cha miaka mitano na faini ya Tsh Milioni saba, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela jana alikuwepo uwanjani kushuhudia vijana wake wakipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza baada ya mchezo huo, Mwakalebela alisema, waliahidi kupata matokeo jana na wamefanikisha
Aidha Mwakalebela amesisitiza ahadi ya kushinda mataji matatu msimu huu iko palepale na sasa wanatangulia mkoani Kigoma tayari kwa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba ambao utapigwa Julai 25
"Tuliwaahidi Wananchama na Mashabiki wetu kuwa msimu huu tumepania kushinda mataji matatu. Tulichukua Mapinduzi Cup, kwenye ligi bado tuko katika mbio za ubingwa na FA tumeingia fainali"
"Ninachowaambia Wanayanga endeleeni kuiunga mkono timu yetu kwani tumedhamiria hatutawaangusha. Tunawaalika kule mkoani Kigoma sisi tunatangulia," alisema Mwakalebela
Ukitaja jina la Mwakalebela wengi wanakumbuka juu ya msimamo wake katika kesi ya Bernard Morrison ambaye jana alifichwa na kijana mdogo kabisa, Kibwana Shomari
Habari njema ni kuwa kesi hiyo ipo, na maamuzi yatatolewa kabla ya mwezi huu kumalizika
Wengi wanajiuliza jeuri ya Yanga kudai wanaweza kutwaa ubingwa inatoka wapi? Tusubiri...!