Wengi wamemchagua mlinzi wa kulia Kibwana Shomari kuwa nyota wa mchezo wa leo dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 lililowekwa kambani na Zawadi Mauya
Kibwana aliwadhibiti mawinga wote waliojaribu kupita upande wake, zaidi Bernard Morrison ambaye kabla ya mchezo huo mashabiki wa Simba walikuwa wakitamba kuwa hazuiliki
Dominic Albinus Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi amempongeza Kibwana kwa kazi nzuri aliyofanya leo
"Hongera sana kijana kwa kazi nzuri sana uliyoifanya leo, hakika unazidi kuwadhihirishia watu kuwa mpira ni akili na sio kimo au mwili mkubwa"
"Wewe ni hazina ya Taifa, ulichokifanya Leo kwa kuwaficha mawinga wote waliocheza upande wako na ukabaji wako wa akili ndio silaha yako," ulisomeka ujumbe wa Albinus
Kwa hakika Kibwana alikuwa katika kiwango bora sana leo, yeye na wachezaji wenzake wamepambana kwa muda wote kupata matokeo haya