Ushindi wa mabao 3-0 iliyopata Azam FC dhidi ya Stand United umeiwezesha timu hiyo kuiondosha Simba kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom japo inaweza kuwa kwa masaa 24.
Mabao ya Salmin Hozza, Benard Arth na Bruce Kangwa yameihakikishia Azam FC alama tatu muhimu zilizopelekea wana rambaramba hao kufikisha alama 26.
Simba ina nafasi ya kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kama itapata ushindi dhidi ya Ndanda FC katika mchezo utakaopigwa kesho Jumamosi, Disemba 30.
Stand United inaendelea kuburuza mkia ikiwa imejikusanyia alama saba pekee
Yanga iliyo nafasi ya tatu na alama 21 itashuka kweye dimba la CCM Kirumba keshokutwa Jumapili, Disemba 31 kuikabili timu ngumu ya Mbao FC.
Kikosi cha Yanga tayari kiko jijini Mwanza kikiendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo

ADVERTISE HERE