Bao la shuti la nje ya 18 lililopigwa na Zawadi Mauya kwenye dakika ya 12 limetosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya watani zao Simba
Kabla ya mchezo huo, kama ilivyo kawaida yao, mashabiki wa Simba walitawala mitandao ya kijamii kwa tambo wakiongozwa na msemaji wao Haji Manara
Hata hivyo Yanga ilijiandaa kimbinu zaidi kucheza mchezo huo, hongera kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa kazi nzuri ya kuhakikisha Yanga inaondoka na alama zote tatu
Yanga imeandika historia zaidi kwa kuendelea kuwanyanyasa watani zao mbele ya Marais wa nchi
Leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan alikuwepo uwanjani kushuhudia mtanange huo
Ni kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo Yanga ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba mbele ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dk John Magufuli
Ni ushindi wa 38 Yanga inapata dhidi ya Simba, lakini ni ushindi uliopeleka heshima kubwa Jangwani
Simba waliamini leo watashinda na pengine kutangazwa kuwa mabingwa, lakini hawakujua Yanga sio timu ya kutumia kama daraja