Nyota wanne kuikosa Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jul 2021
Nyota wanne kuikosa Simba

Kocha wa makipa Yanga Razack Siwa amesema maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi, Julai 03 yamekamilika

Akizungumza na Wanahabari katika Mkutano wa mechi, Siwa amesema timu iko tayari na wamepania kushinda mchezo huo

"Hakuna mtu asiyejua derby ya Simba na Yanga ilivyo, hakuna haja ya kuhamasishana sana lakini sisi tumejiandaa kupata ushindi," alisema Siwa

Aidha Siwa amesema nyota wanne watakosekana kutokana na sababu mbalimbali

"Tuna wachezaji wanakosekana kutokana na changamoto za hapa na pale, Haruna Niyonzima ni mgonjwa wakati Lamine Moro na Michael Sarpong wana majeraha. Pia Mapinduzi Balama yeye bado hajaanza mazoezi na timu"

"Wachezaji Abdallah Shaibu 'Ninja' na Yassin Mustafa wameshaanza mazoezi nasi hivyo wako tayari kuelekea mchezo huo," alisema Siwa

Nae nahodha Msaidizi Abdallah Shaibu 'Ninja' amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo, wamejiandaa kuibuka na ushindi

"Tunamshukuru Mungu sote mimi na wachezaji wenzangu tuko salama. Tuko tayari kucheza na Simba, hatuangalii kama ni mchezo wa kwanza au wa ngapi, hatutakubali kufungwa na Simba," alisema Ninja

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
57m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’