Mara nyingi mechi dhidi ya Simba zinazopigwa uwanja Benjamin Mkapa hasa Simba wanapokuwa wenyeji, malalamiko ya 'harufu' vyumbani huwa hayakosekani
Sasa kuelekea mchezo wa kesho, kutakuwa na ukaguzi maalum vyumbani kulingana na Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz
Aidha Nugaz amesema pia wachezaji wote watapimwa afya zao kabla ya mchezo
"Tunaishukuru sana Serikali, kwani kwa mara ya kwanza kabla ya mchezo wachezaji watapimwa. Lakini sio kupimwa tu pia vyumba vyote vitakaguliwa, hakuna janjajanja tena", alisema Nugaz katika mahojiano na EFM
Mara kadhaa imeshuhudiwa katika michezo iliyopita Yanga ikigoma kuingia vyumba vya kubadilishia nguo inapocheza na Simba kutokana na harufu kali inayotoka katika vyumba
Tatizo hili hutokea wakati tu Simba inapokuwa mwenyeji wa mchezo kama utakavyokuwa mchezo wa kesho