Wananchi Yanga wanaendelea kujiweka sawa Kigamboni kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya watani zao Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga inakamilisha maandalizi yake ya mwisho leo kuelekea mchezo huo ambao hesabu za Wananchi ni kuondoka na alama zote tatu
Habari njema ni kurejea kikosini kwa walinzi Abdallah Shaibu 'Ninja' na Yassin Mustafa ambao walikosekana kwa takribani wiki nane wakiwa majeruhi
ADVERTISE HERE