Kwa Yacouba, Kisinda, Feisal hawatoki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jul 2021
Kwa Yacouba, Kisinda, Feisal hawatoki

Winga wa zamani wa Yanga, mkongwe Edibily Jonas Lunyamila amesema mchezo wa kesho dhidi ya Simba hautakuwa mwepesi kwa kila timu

Pamoja na kuiona Simba kuwa na kikosi bora zaidi kuelekea mchezo huo, Lunyamila amesema bado anaipa nafasi Yanga kuweza kuibuka na ushindi kutokana na kasi ya safu ya ushambuliaji

"Mechi itakuwa ngumu kwa pande zote mbili, lakini timu ambayo itatengeneza nafasi nyingi itakuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi"

"Simba ni wazuri, wana wachezaji wenye uwezo mkubwa, lakini naipa nafasi Yanga kuibuka na ushindi kutokana na ukali wa safu yake ya ushambuliaji ikiongozwa na kina Tuisila Kisinda, Feisal Salum na Yacouba Sogne," alisema Lunyamila

"Siku za karibuni naona safu ya ushambuliaji imekuwa bora, wana kasi na ushirikiano mzuri katika kutengeneza mashambulizi"

"Mabeki wote wa Simba hawana kasi kama ilivyo kwa washambuliaji wa Yanga, kwa hiyo kama Yanga itapiga presha mara tatu kutokana na kasi yao lazima watapata bao kwani mechi ya kwanza iliyoisha kwa sare Kisinda alifanya safari moja tukapata penalti," aliongeza Lunyamila

Hata hivyo,Lunyamila ametoa tahadhari kwa safu ya ulinzi ya Yanga inapaswa kuwa makini sababu wapinzani wao Simba wana wachezaji wengi hatari, akiwemo nahodha wao, John Bocco na Luis Miquissone

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’