Tunawasubiri Benjamin Mkapa - Bumbuli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jul 2021
Tunawasubiri Benjamin Mkapa - Bumbuli

Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Jumamosi, Julai 03 uwanja wa Benjamin Mkapa yanakwenda vizuri

Bumbuli amesema wanauchukulia mchezo dhidi ya Simba kama ilivyo michezo mingine tu, hivyo hawana hofu yoyote

Aidha Bumbuli amesema wachezaji Abdallah Shaibu 'Ninja' na Yassin Mustafa wamerejea kikamilifu kikosini baada ya kupona majeraha yaliyowaweka nje kwa takribani wiki nane

Amesema wachezaji hao wako tayari kwa mtanange wa Jumamosi, kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anaweza kuwajumuisha kwenye kikosi chake

Bosi huyo wa kitengo cha habari amesema wao hawatakuwa na maneno mengi lakini wanawasubiri uwanja wa Benjamin Mkapa hapo kesho

"Maendeleo yetu ni mazuri, na wachezaji wetu Abdallah Shaibu Ninja na Yassin Mustapha waliokuwa majeruhi kwa takribani wiki nane wamerejea"

"Hivyo kutakuwa na chaguo pana kwa benchi la ufundi katika nafasi ya ulinzi. Hii ni mechi ya kawaida kama zilivyo mechi zingine, kwani wachezaji wanacheza (11) kila upande, isipokuwa hii ni mechi ya watani wa jadi, na wenzetu watakuwa na presha kubwa kuliko sisi kwa sababu wanataka kutangaza ubingwa katika mechi yetu," alisema Bumbuli

"Kuhusu Manara kuwaomba (TFF) walete kombe uwanjani yale ni maneno tu, nasisi tukiamua kuongea tunamaneno makali. Bila makandokando hawawezi kutufunga na zile goli nne anazosema walitufunga ni kwa sababu kimazingira kulikuwa na baadhi ya wachezaji wetu kuwa upande wao"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
31m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’