Mzee Mpili amejizolea umaarufu siku karibuni kutokana na misimamo yake linapokuja jambo lolote linaloihusu Yanga
Juzi alipata mwaliko kuonana ana kwa ana na viongozi wa Yanga na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambapo pamoja na mambo mengine aliwapa ahadi moja tu, kuwa wao waiandae timu vizuri ushindi ni uhakika Jumamosi
Kuhusu ile michezo yao ya 'paka weusi' Mzee Mpili akawaambia wala wasiwe na wasiwasi kwani nao wanao watu na watashusha nyuklia siku hiyo
Tunawatahadharisha tu, Mzee Mpili ndio kaondoka Ikwilili Rufiji anaelekea jijini Dar es salaam akiwa na silaha zote!
Sasa waende wakafanye miujiza yao pale kwa Mkapa, wataumbuka mchana kweupeee...!
ADVERTISE HERE