Sasa ni wakati wa utekelezaji - Senzo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jun 2021
Sasa ni wakati wa utekelezaji - Senzo

Siku moja baada ya wanachama wa klabu ya Yanga kupitisha kwa asilimia 100 rasimu ya mabadiliko ya Katiba na muundo wa uendeshaji wa klabu hiyo, mshauri wa Yanga, Senzo Mazingiza amesema kazi kubwa iliyokuwa mbele yao ni kuhakikisha wanatimiza yale waliyoahidi

Yanga imepania kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo ili kuachana na utegemezi wa fedha kutoka mfukoni kwa mtu mmoja na kujitegemea kwa mfumo wa uwekezaji na kampuni.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Senzo alisema sasa ni wajibu wao kama kamati kuhakikisha wanayatimiza yale yote ambayo waliahidi ili kuwapa furaha wanachama na mashabiki wa Yanga.

Mshauri huyo alisema huu ndio wakati sahihi wa kuanza kuyafanyia kazi masuala hayo, kila kiongozi kwa wakati wake anatakiwa kuwajibika kwa kupigania maendeleo ya klabu hiyo sababu endapo watafanikisha waliyokusudia anaami timu hiyo itakuwa ya kupigiwa mfano.

Alisema pamoja na yote ana imani kubwa na uongozi wa Mwenyekiti, Dk Mshindo Msolla kwamba kama ilivyokuwa mwanzo wakati wanaanza mchakato huo; watapambana na kuhakikisha malengo yao yanafanikiwa na kuifanya Yanga timu ya kipekee kuanzia ndani na nje ya Tanzania.

Senzo alisema uendeshwaji wa mpira umebadilika duniani kote na mabadiliko ambayo wameyafanya yatabadilisha mpira wa Tanzania na kuvishawishi vilabu vingi vya Tanzania na nchi za jirani kuiga uendeshwaji huo

Kiongozi huyo amewashukuru wanachama wa Yanga kwa kuonesha imani kubwa kwa kamati iliyofanikisha jambo hilo na yeye ameahidi kuwapambania hadi siku ya mwisho ili kuona mchakato huo unakamilika na Yanga inaendeshwa kisasa kama ilivyo baadhi ya klabu Afrika na Ulaya.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’