Tayari Wanachama wa Yanga wameridhia timu yao kubadili muundo wa uendeshaji wakielekea kwenye Mabadiliko
Injinia Hersi Said ambaye ni Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano amesema mchakato wa kuelekea kwenye Mabadiliko ndio unaanza sasa
Hersi amesema wanakwenda kufungua mipaka ya umiliki wa klabu ambapo wataanza kwa kufanya tathmini ya thamani ya klabu ili kupanga utaratibu na bei ya hisa
"Hatua ya kwanza ya Mabadiliko ya Katiba imekamilka, kinachofuata sasa baada ya wanachama kukubali mabadiliko ni kufungua mipaka ya umiliki wa klabu, tutafanya tathmini ya thamani ya klabu ili kuamua hisa zitauzwaje," alisema Hersi
Kampuni ya Yanga itauza hisa asilimi 49% kwa wawekezaji na asilimia 51% zitamilikiwa na Wanachama
Wawekezaji watatu hadi wanne watauziwa hisa hizo ambapo ili Mwekezaji kuwa na Uwakilishi kwenye Bodi anapaswa kuwa na hisa kuanzia asilimia 12%
Bodi ya Yanga itakuwa na Wajumbe tisa, Wajumbe watano kutoka Yanga na Wajumbe wanne kutoka kwa Wawekezaji