Baada ya Mkutano wa jana 27/06/2021 maana yake sasa Yanga inaelekea kwenye Mabadiliko ya Kimfumo
Hivyo basi wanayanga wote wanapaswa kujiandaa kuwa wanachama na hata mashabiki pia kwa utaratibu ulioainishwa
KUWA MWANACHAMA
1). Kila tawi litakuwa na fomu ambayo itajazwa na mwanachama. Fomu hiyo itapatikana kwa gharama ya shilingi 2,000/= Fomu hii itawasilishwa Makao Makuu ya Klabu na Viongozi wa Tawi.
Pesa ya fomu utakayolipa itabakia kwenye tawi lako ili itumike kwa kazi za tawi
2). Baada ya kujaza fomu utalipia pia kadi yako kwa shilingi 5,000/= Kadi hii itakuwa imekupa sifa ya Kuwa Mwanachama mwenye kadi ambaye anasifa za kuchagua na kuchaguliwa
3). Ukishapata kadi yako utalipa ada ya Mwaka mzima kwa shilingi 24,000/= sawa na shilingi 2,000/= kwa kila mwezi
Hivyo basi gharama ya Jumla ya kuwa mwanachama kwa mfumo mpya ni shilingi 31,000/=
Aidha kwa siku za usoni kutakuwa na faida a kuwa mwanachama ambazo zitahusisha mambo mengi, mfano kuingia viwanjani, kulipia usafiri, kupata jezi n.k
KUWA SHABIKI
1. Kuwa mshabiki wa Yanga unaweza kupitia kwenye tawi au online kwa Internet au App ambayo utaijaza kwa Simu yako.
2. Baada ya kujisajiri kupitia tawi au online utalipia pia kadi yako kwa shilingi 5,000/= Kadi hii sasa itakuwa imekupa sifa ya Kuwa Mshabiki mwenye kadi ambaye hana sifa za kuchagua au kuchaguliwa.
3. Ukishapata kadi yako pia utalipa ada ya Mwaka mzima kwa shilingi 12,000/= sawa na shilingi 1,000/= kila mwezi.
Hivyo basi gharama ya kuwa mshabiki kwa mfumo mpya ni shilingi 19,000/=. Kwa siku za usoni kutakuwa na faida ya kuwa mshabiki ambazo zitahusisha mambo mengi mfano kuingia viwanjani, kulipia usafiri, kupata jezi n.k.
KADI ZA WATOTO
Kadi za watoto zitalipiwa shilingi 5,000/= bila ada za mwezi kwakuwa watoto hawana kipato bali lengo ni kumuandaa kuwa Mwanachama au Mshabiki kwa siku za usoni