Jiandae kuwa Mwanachama au shabiki wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jun 2021
Jiandae kuwa Mwanachama au shabiki wa Yanga

Baada ya Mkutano wa jana 27/06/2021 maana yake sasa Yanga inaelekea kwenye Mabadiliko ya Kimfumo

Hivyo basi wanayanga wote wanapaswa kujiandaa kuwa wanachama na hata mashabiki pia kwa utaratibu ulioainishwa

KUWA MWANACHAMA

1). Kila tawi litakuwa na fomu ambayo itajazwa na mwanachama. Fomu hiyo itapatikana kwa gharama ya shilingi 2,000/= Fomu hii itawasilishwa Makao Makuu ya Klabu na Viongozi wa Tawi.

Pesa ya fomu utakayolipa itabakia kwenye tawi lako ili itumike kwa kazi za tawi

2). Baada ya kujaza fomu utalipia pia kadi yako kwa shilingi 5,000/= Kadi hii itakuwa imekupa sifa ya Kuwa Mwanachama mwenye kadi ambaye anasifa za kuchagua na kuchaguliwa

3). Ukishapata kadi yako utalipa ada ya Mwaka mzima kwa shilingi 24,000/= sawa na shilingi 2,000/= kwa kila mwezi

Hivyo basi gharama ya Jumla ya kuwa mwanachama kwa mfumo mpya ni shilingi 31,000/=

Aidha kwa siku za usoni kutakuwa na faida a kuwa mwanachama ambazo zitahusisha mambo mengi,  mfano kuingia viwanjani, kulipia usafiri, kupata jezi n.k

KUWA SHABIKI

1. Kuwa mshabiki wa Yanga unaweza kupitia kwenye tawi au online kwa Internet au App ambayo utaijaza kwa Simu yako.

2. Baada ya kujisajiri kupitia tawi au online utalipia pia kadi yako kwa shilingi 5,000/= Kadi hii sasa itakuwa imekupa sifa ya Kuwa Mshabiki mwenye kadi ambaye hana sifa za kuchagua au kuchaguliwa.

3. Ukishapata kadi yako pia utalipa ada ya Mwaka mzima kwa shilingi 12,000/= sawa na shilingi 1,000/= kila mwezi.

Hivyo basi gharama ya kuwa mshabiki kwa mfumo mpya ni shilingi 19,000/=. Kwa siku za usoni kutakuwa na faida ya kuwa mshabiki ambazo zitahusisha mambo mengi mfano kuingia viwanjani, kulipia usafiri, kupata jezi n.k.

KADI ZA WATOTO

Kadi za watoto zitalipiwa shilingi 5,000/= bila ada za mwezi kwakuwa watoto hawana kipato bali lengo ni kumuandaa kuwa Mwanachama au Mshabiki kwa siku za usoni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’