Afisa Mshamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema baada ya Wanayanga kufanikisha Mabadiliko, sasa wanaelekeza nguvu kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi, Julai 03 uwanja wa Benjamin Mkapa
Nugaz amesema watashuka dimbani kucheza mchezo huo wanachoomba yasitokee mabadiliko kama ilivvyokuwa May 08
"Sisi tuko tayari, hata wakituamsha saa sita usiku tunacheza. Tunachoomba tu waje uwanjani wasifanye ujanja ujanja kama mchezo uliopita," alisema Nugaz
Aidha Nugaz amesema pia wataandaa utaratibu kwa mashabiki kwenda kuiunga mkono timu yao mkoani Kigoma kwenye mchezo wa fainali kombe la FA utakaopigwa Julai 25
Yanga na Simba zitakutana mara tatu katika kipindi cha miezi miwili
Kutakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa Mwezi August