Pamoja na changamoto walizopitia, uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla wamekuwa na nidhamu kubwa kwenye matumizi ya fedha
Tangu mwaka 2019, Yanga imejiendesha ndani ya bajeti yake huku ikibaki na ziada
Bajeti ya mwaka 2019 fedha zilizopatikana ni Tsh Bilioni 4.683 na matumizi Tsh Bilioni 4.678, Yanga ikafunga mwaka na ziada ya Tsh Milioni 5 zilizobaki
Bajeti ya mwaka 2020, Yanga ilikusanya Tsh Bilioni 5.857, matumizi Tsh Bilioni 5.731 na kubaki na ziada ya Tsh Milioni 126
Bajeti ya mwaka 2021, fedha zilizokusanywa ni Tsh Bilioni 8.149, matumizi ni Tsh Bilioni 7.984 na kubaki na zaida ya Tsh Milioni 164
Kwa mwaka wa fedha 2021/22, Yanga imetenga jumla ya Tsh Bilioni 8. 1Β
Kitita cha Tsh Bilioni 4.9 kwa ajili ya kulipa mishahara na Tsh Milioni 854.7 kwa ajili bonus
Yanga inatarajia kukusanya kitita cha Tsh Bilioni 8.1, na matumizi yake itakuwa Tsh Bilioni 7.9
GSM wanaendelea kuhusika na usajili kwa asilimia 100% pamoja na kambi za timu na gharama nyingine za uendeshaji wa klabu. Jukumu la Yanga ni kulipa mishahara ya wachezaji