Maneno ya shukrani kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa uwekezaji GSM
Ni baada ya Wanachama kufanya Mabadiliko ya Katiba yanayokwenda kuruhusu Mabadiliko ya mfumo wa Uendeshaji
Imekuwa safari ndefu yenye milima, mabonde, jua kali, mvua nyingi ila hatimaye tumefika safari yetu kuelekea mabadiliko katika klabu yetu.
Ilianza kwa kuwa katika ILANI ya UCHAGUZI ya M/Kiti Dr. Mshindo Msolla na hatimaye kuunda kamati ya mabadiliko chini ya mwanasheria msomi ALEX MGONGOLWA.
Kazi kubwa ilifanyika na kwa USHAURI mkubwa wa LALIGA katika kupitia mfumo imara ( STABLE ), wa muda mrefu ( LONG TERM ), wenye malengo mazuri ( RESULT ORIENTED ) na wenye uhalisia wa kitanzania ( CUSTOMIZED ).
Maeneo yaliofanyiwa kazi katika mabadiliko haya ni kama yafuayo;
1. Umiliki wa klabu - CLUB OWNERSHIP
2. Muundo wa klabu - STRUCTURE OF ADMINISTRATION.
3. Ushirikishwaji wa wanachama na mashabiki - FAN ENGAGEMENT
Aidha, kuelekea kwenye mabadiliko ya klabu, yako maeneo mengine yatahitaji kupitiwa kupitia dirisha la mabadiliko.
1. Football development
2. Legal and complience
3. Financial controls
4. Marketing
5. Communication
6. Sales
Mfumo huu uliopitishwa leo unaenda kuwa mfumo bora barani AFRICA na wa kuigwa na vilabu vingine.
Kwa umuhimu wa kipekee niishukuru sana KAMATI YA MABADILIKO YA KATIBA iliundwa ili kuweza kuyabeba mabadiliko hayo.
Elimu kwa wanachama kupitia matawi na vikundi maalum vilipata nafasi ya kujifunza mfumo na kutoa mapendekezo yao ambayo leo hii yanakwenda kuijenga YANGA MPYA.
Hakika leo HISTORIA IMEANDIKWA!!!
Shukran za kipekee ziwafikie wafuatao;
1. Dr. Mshindo msola, Kamati ya utendaji na sekretarieti - Kupitia uongozi wao, leo YANGA imekwenda kwenye mfumo mpya.
2. ALEX MGONGOLWA na RAYMOND WAWA - Wenyeviti wa kamati ya MABADILIKO & KATIBA.
3. Wanachama, wapenzi na mashabiki wa klabu hii KONGWE kwa kutoa BARAKA zao kuelekea mabadiliko ya mfumo.
Kwa umuhimu wa kipekee, nimshukuru sana Mr. GHALIB SAID MOHAMED kwa jitihada za dhati kabisa kwenye kuijenga YANGA hii.
Ukiachilia mbali mengi mazuri kupitia kujitoa kwake, hili la MABADILIKO limekuwa ni la kipaumbele sana. YANGA yetu ya kesho iko mikononi mwa MFUMO WA KISASA.
Hakika historia itawataja vyema!!