Katika Mkutano Mkuu wa Wanachama leo, uongozi wa Yanga kupitia Kamati yake ya Miundombinu, waliwaonyeshwa Wanachama aina ya uwekezaji unaokwenda kufanyika kule Kigamboni
Katika eneo lake la ekari saba, Yanga itajenga Kituo cha michezo ambacho kitakuwa na kila kitu ndani
Hosteli ambayo itakuwa na vyumba 28, viwanja viwili, Gym,Β swimming pool, ofisi na mahitaji yote muhimu kwa ajili ya timu ya mpira wa miguu
Aidha kiwanja kitakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki kati ya 700 hadi 1000 ambao wanaweza kuingia kushuhudia mazoezi ya timu
Ni mradi wa kisasa ambao utaweka historia kwa klabu za soka hapa Tanzania
ADVERTISE HERE