Tutajenga timu bora Afrika - GSM

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jun 2021
Tutajenga timu bora Afrika - GSM

Wadhamini wa klabu ya Yanga kampuni ya GSM imeahidi kuendelea kuisaidia Yanga kuhakikisha inakuwa timu yenye ushindani na mafanikio Afrika

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa GSM Galib Said Mohammed 'GSM', Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni hiyo, Injinia Hersi Said, amesema wataendelea kuipigania Yanga bila ya kujali watakuwa miongoni mwa wawekezaji au la

Injinia Hersi amesema msimu huu GSM wamewekeza fedha nyingi katika usajili unaolenga kuliteka soka la Afrika

"Wakati tunaingia Yanga tulikuwa na mipango ya mda mfupi na mda mrefu, tunashukuru chini ya mwenyekiti Dr. Mshindo Msolla tumeweza kuinua thamani ya Klabu, mpango wa mda mrefu ni kuhusu mabadiliko ya Klabu yetu ambao haki ya Wanachama wetu imezingatiwa kwa kuwashirikisha"

"Tunashukuru kuwa sehemu ya Familia ya Yanga na tayari tumeanda fedha kwa ajili ya kufanya usajili wa nguvu, ambao itatufanya kuwa timu bora ndani na nje ya Afrika," alisema Injinia

Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji imeteuwa Wajumbe watano wa Baraza la Wadhamini

Dk Msolla amewataja Wajumbe hao kuwa ni George Mkuchika,  Geofrey Mwambe , Abbas Tarimba, Mama Fatma Karume na Mwigulu Nchemba

Aidha Kamati ya Utendaji pia imewafungulia Wajumbe watatu waliokuwa wamefungiwa kutokana na sababu mbalimbali

"Katika kuzingatia kuleta umoja ndani ya Klabu Wajumbe watatu waliokuwa wamesimamishwa mwaka jana wamerudishwa kwenye nafasi zao kuendelea kwenye majukumu yao"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’