Ni mchezo wa tatu kocha Nasreddine Nabi amemtumia kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' eneo la kiungo mchezeshaji
Mchezo wake wa kwanza ulikuwa dhidi ya Ruvu Shooting akifanikiwa kufunga mabao mawili
Akatumika tena kwenye eneo hilo katika mchezo dhidi ya Mwadui Fc akaisaidia Yanga kupata ushindi wa mabao 3-2
Kwa mara nyingine Nabi leo amemtumia katika nafasi hiyo na amechangia Yanga kuondoka na ushindi muhimu dhidi ya Biashara United
Pasi yake murua katika dakika ya 22 ilitumiwa vyema na Yacouba Songne kuifungia Yanga bao lililowapeleka fainali
Fei Toto anastahili kuwa nyota wa mchezo leo kwani alihusika katika kila shambulizi la hatari ambalo Yanga walifanya
Alitoa pasi nne za hatari, akiwatengenezea Yacouba (2), Tuisila na Saido
Taratibu ameanza kuyazoea majukumu yake mapya, sasa Yanga imeanza kuonyesha sura tofauti inaposhambulia
Nabi amemwamini Fei Toto kwa kumchezesha nafasi ambayo wenzake waliopita walishindwa kubaini faida yake