Yanga imepigana vita ya kiume kuweza kutinga fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuichapa Biashara United bao 1-0
Ulikuwa mchezo ambao kocha Nasreddine Nabi alihitaji matokeo zaidi kuweza kuipeleka Yanga fainali yake ya kwanza baada ya miaka mitano
Yanga imetinga fainali katika michuano ambayo asilimia 90 ya mechi zake wamecheza mikoani
Mchezo pekee ambao Yanga walicheza jijini Dar es salaam ni dhidi ya Kengold
Kuweza kutinga fainali kwa kushinda mechi nyingi zilizopigwa katika viwanja vyenye changamoto, haikuwa kazi rahisi
Yanga sasa iko fainali na kwa hakika vijana wako tayari kulipeleka taji la FA Jangwani
Mchezo wa fainali utapigwa uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma
Iwe Simba au Azam Fc, huko mkoani Kigoma hakuna atakayetoka salama..!