Wananchi wameingia zao fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuichapa Biashara United bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora
Yacouba Songne ameendeleza moto ya kupasia nyavu akifunga bao pekee la Yanga katika dakika ya 22
Ni baada ya pasi murua kutoka kwa Feisal Salum 'Fei Toto'. Yacouba alipokea pasi kutoka kwa Mukoko Tonombe, akamuwekea moja Feisal ambaye nae bila ya ajizi akamtengea Yacouba pasi ya bao



Yanga ilikuwa hatari zaidi kwenye kipindi cha kwanza, Tuisila Kisinda akikosa nafasi nyingine ya bao
Biashara United walikuja juu kwenye kipindi cha pili lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Yanga ikiongozwa na nahodha Bakari Nondo, Dickson Job, Kibwana Shomari na Adeyum Saleh, walihakikisha wanaulinda ushindi huo wa Yanga
Baada ya kukosekana hatua ya fainali kwa takribani miaka mitano, Wananchi wametangulia mapema sasa wakimsubiri mshindi wa mchezo kati ya Azam Fc dhidi ya Simba utakaopigwa kesho mkoani Ruvuma