Jioni ya leo kikosi cha Yanga kitashuka uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora kuikabili Biashara United katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Wananchi wako mkoani Tabora tangu juzi, jana wakifanya mazoezi yao ya mwisho uwanja wa Ali Hassan Mwinyi
Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga kuhakikisha wanashinda ili kutinga fainali
Yanga iliweka malengo makubwa msimu huu, kushinda taji la FA ni moja ya malengo yake
Kocha Razak Siwa amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa tisa na nusu Alasiri
Yanga ilipata mapokezi makubwa mkoani Tabora na bila shaka jioni ya leo mashabiki wake watajitokeza kwa wingi kuwaunga mkono vijana wao
Ikumbukwe mwishoni mwa wiki hii Yanga itakuwa na tukio la kihistoria ambapo Mkutano Mkuu wa Wanachama utafanyika kupitisha Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji
Ushindi dhidi ya Biashara United utanogesha shamrashamra za Wananchi kuelekea tukio hilo
Ni saa tisa na nusu Alasiri pale dimba la Ali Hassan Mwinyi..