Viongozi waandamizi wa Yanga wameendelea kuaminiwa kwa kupewa nafasi kubwa za uongozi Tanzania Bara na kule Visiwani Zanzibar
Ni baada ya Arafat Ally Haji, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa kamati ya Fedha na Mipango Klabu ya Yanga, kuteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC)
Taarifa ya uteuzi wa Arafat ilitangazwa mapema leo na Ikulu ya Zanzibar
Wanayanga tunamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya
ADVERTISE HERE