Jumapili, Juni 27 itakuwa siku ya kihistoria kwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jun 2021
Jumapili, Juni 27 itakuwa siku ya kihistoria kwa Yanga

Jumapili ya wiki hii Juni 27 2021, Wanachama wa klabu ya Yanga wanakwenda kuandika historia ambapo kupitia Mkutano Mkuu, watafanya marekebisho ya Katiba ili kuruhusu mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu ya Yanga

Kwa miaka 86, Yanga imemilikiwa na Wanachama kwa asilimia 100 lakini sasa muundo huo unakwenda kubadilika kwa kuunda kampuni ambayo asilimia 49% ya hisa, zitauzwa kwa Wawekezaji watatu au wanne

Uongozi wa Yanga wakiongozwa na Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla, GSM ambao wamejitolea kugharamia mchakato huo, wanastahili pongezi za dhati kwa hatua hiyo muhimu

Kwa wasiofahamu Yanga ilianza vuguvugu la Mabadiliko ya kiuendeshaji tangu mwishoni mwa miaka ya 90

Hata hivyo, kuliibuka na vikwazo vingi kufanikisha Mabadiliko hayo. Mara nyngi yamejitokeza makundi ambayo kwa maslahi yao, wanapinga Mabadiliko ya mfumo kwa hofu ya kupoteza 'ulaji'

Mbunge wa Kinondoni, Mh Abbas Tarimba anakumbuka jinsi Yanga iliosambaratika mwishoni mwa miaka ya 90 baada ya kuibuka kwa mgogoro wa Yanga Asili na Yanga Kampuni

Tarimba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Yanga wakati huo, amesema hitaji la Mabadiliko katika usimamizi na uendeshaji wa klabu kutokana na hali halisi halikuanza leo

"Wakati wa uongozi wetu kulikuwa na mgogoro baina ya klabu na wafadhili, aliyekuwa Katibu Mkuu, George Mpondela 'Castro' ndipo akaja na wazo la Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu"

"Mpondela alileta wazo la kampuni baada ya wafadhili kujiondoa. Kwa bahati mbaya alishindwa kuliendesha wazo lake kutokana na migogoro. Tulilipokea wazo na tukaona tutengeneze mfumo wa klabu kujiendesha lengo ni kuachana na wafadhili waliokuwa wakituyumbisha"

"Tulikwenda kwenye Matawi yote, kwa ajili ya kuwaelimisha wanachama Mabadiliko na kuwapa nafasi ya kuuliza maswali ili waweze kukifahamu kile ambacho tunakilenga. Hapo ndipo ulipoibuka mgogoro wa Yanga Asili na Yanga Kampuni, kwamba Kampuni walikubali na Asili hawakutaka Mabadiliko chini ya Mzee Yusuf Mzimba

"Chanzo kikubwa ni mgongano wa kimaslahi kwa baadhi ya watu ndani ya klabu, ni tamaa tu ya watu wachache ambao waliamini iwapo mabadiliko yatafanyika, hawatapata nafasi ya kupata masilahi binafsi ndani ya klabu," alisema Tarimba

Lakini wakati huu Yanga chini ya Dk Msolla na kwa usaidizi wa GSM, wamepiga hatua zaidi na wanakaribia kufanikisha ndoto ya akina marehemu Mpondela waliyokuwa nayo tangu miaka ya 90

Wananchama wamepewa elimu ya kutosha na bila shaka Mkutano Mkuu utatumika kuivusha Yanga katika hatua muhimu zaidi yenye mafanikio

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’