Wananchi hawataki 'mbeleko' Kimataifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jun 2021
Wananchi hawataki 'mbeleko' Kimataifa

Yanga iko Tabora wakisubiri kushuka uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kuikabili Biashara United katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)

Mchezo huo utapigwa kesho Ijumaa, ukitarajiwa kuanza saa tisa na nusu Alasiri

Yanga imedhamiria kuibuka mabingwa wa michuano hiyo hivyo hesabu ni kushinda mhchezo huo wa nusu fainali

Wananchi wameweka wazi kuwa wanataka kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao kwa jasho lao wenyewe

Razak Siwa ambaye ni mkufunzi wa makipa wa Yanga amesema, wametua Tabora wakiwa na lengo moja la kusaka ushindi dhidi ya Biashara United

"Hatutaki kupoteza katika mchezo huu, lazima tupambane kutafuta matokeo mazuri, malengo yetu ni kushiriki michuano ya kimataifa kwa nguvu zetu, tunahitaji matokeo ya ushindi katika mchezo huu kwa ajili ya fainali," alisema Siwa

Yanga imepoteza matumaini ya kushinda ubingwa wa ligi kuu na sasa nguvu zote zimeelekezwa kwenye michuano ya FA

Tayari Wananchi wana tiketi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao lakini wanahitaji kushinda taji la FA kumaliza msimu na angalau kombe hilo ambalo pia litawapa tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’