Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano klabu ya Yanga Injinia Hersi Said leo ameshiriki tukio la uzinduzi wa Tawi la Yanga mkoani Tabora linalofahamika kama Yanga Kwanza
Katika tukio hilo, Hersi amemwakilisha Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla
Yanga iliwasili mkoani Tabora mapema leo kuelekea mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Biashara United utakaopigwa keshokutwa Ijumaa, uwanja wa Ali Hassan Mwinyi




ADVERTISE HERE