Waziri wa Fedha Mh Dk Mwigulu Nchemba ni Mwanayanga 'lialia' na leo wakati akihitishisha mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Fedha kule Bungeni mkoani Dodoma, alichomekea kidogo masuala ya utani waj adi
Pamoja na kuwapongeza Simba kwa kufika robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa, Dk Mwigulu aliishangaa timu hiyo kwa kutoshukuru 'upendo' wa Yanga baada ya kuachiwa mchezaji Barnard Morrison
Aidha Dk Mwigulu akawataka Wanayanga wasisumbuke na Morrison kwani wanarejeshewa mshambuliaji Heritier Makambo
"Wanayanga wameonyesha upendo kwa Simba kwa kuwaachia Bernard Morrison lakini inasikitisha Simba wameshindwa hata kurudisha gharama ya nauli ambayo Yanga walitumia kumleta Morrison hapa nchini"
"Nawaambia Wanayanga endeleeni na upendo huo achaneni na Morrison kwani anakuja Makambo...!," alisema Dk Mwigulu
Tetesi za Makambo kurejea Yanga zimeendelea kutawala magazeti na mitandao ya kijamii pamoja na kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Injinia Hersi Said ambaye anasimamia michakato ya usajili, hajaweka wazi kama Makambo anatua au la
Makambo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Horoya AC ingawa inaelezwa kuwa Horoya wako tayari kumuuza au kumtoa kwa mkopo mshambuliaji huyo raia wa DR Congo
Β