Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kesho Jumatano kuelekea mkoani Tabora kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Biashara United
Mchezo huo utapigwa Ijumaa ya wiki hii katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi
Yanga itaelekea Tabora huku ikiwakosa baadhi ya nyota kutokana na sababu mbalimbali
Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amewataja Mapinduzi Balama, Lamine Moro, Michael Sarpong, Abdallah Shaibu, Yassin Mustafa na Metacha Mnata hawatasafiri
Ninja, Mustafa, Balama, Sarpong na Moro ni majeruhi wakati Metacha alisimamishwa na uongozi wa Yanga
Yanga imepania kutwaaΒ ubingwa wa FA hivyo ushindi katika mchezo dhidi ya Biashara United ni lazima ili kuweza kutinga fainali
ADVERTISE HERE