Kwa mara nyingine jana pacha ya Yacouba Songne na Deus Kaseke iliinufaisha Yanga wawili hao wakishirikiana kupatikana kwa bao la pili ambalo lilikuwa la kusawazisha kwa Yanga katika mchezo dhidi ya Mwadui Fc uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 3-2
Krosi ya Tuisila Kisinda ilitua mguu kwa Kaseke nae akamtengea pacha wake Yacouba ambaye bila ya ajizi akauweka mpira kambani na kufufua matumaini ya Yanga kuondoka na alama zote tatu katika dakika za majeruhi
Wawili hawa pia waliizima Mwadui Fc kule Shinyanga kwenye mchezo wa kombe la FA, Deus Kaseke akifunga bao la pili akipokea pasi murua ya kichwa kutoka kwa Yacouba
Kwa sasa Yacouba na Kaseke ndio wachezaji waliohusika katika mabao mengi zaidi kwenye kikosi cha Yanga msimu huu
Yacouba akifunga mabao tisa (nane ligi, moja FA) na Kaseke akifunga mabao nane (sita ligi, mawili FA)
Kaseke ana pasi sita za mabaoΒ wakati Yacouba ametengeneza mabao matano
Ni hivi nyota hao wanapokuwa uwanjani, wanaongeza uwezekano wa Yanga kufunga
Kwani kama hatafunga Yacouba basi atafunga Kaseke, na kama hawafungi basi watahusika kutengeneza mabao iwe kwa wao wenyewe au kwa wachezaji wengine