Mlinzi wa kulia wa Yanga Kibwana Shomari amesema hana wasiwasi na nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza baada ya taarifa kuwa Yanga imekamilisha usajili wa mlinzi wa AS Vita Shabani Djuma
Kibwana ndiye mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi kwenye kikosi cha Yanga msimu huu. Amekosa mtu wa kumpa changamoto katika nafasi yake ambayo pia anacheza Paulo Godfrey 'Boxer'
Jana katika mchezo dhidi ya Mwadui Fc, kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alimuhamishia Kibwana upande wa kushoto huku Boxer akipewa nafasi ya kucheza dakika 90 kwa mara ya kwanza
Kibwana alisema anafurahia usajili huo kwa kuwa utampa changamoto ya kupambana ili kupata nafasi ya kucheza na kupandisha kiwango chake

"Nasikia Djuma Shabani amesaini Yanga na tutakuwa naye msimu ujao, ni jambo zuri kwa sababu anakuja kuboresha timu yetu na mimi nafurahi sababu nitajifunza vitu vingi kutoka kwake kutokana na uzoefu alionao, lakini sihofii kukosa nafasi ya kucheza sababu mwenye jukumu la kupanga timu ni kocha," alisema Kibwana
Mlinzi huyo ambaye alijiunga na Yanga akitokea Mtibwa Sugar, alisema kucheza nafasi moja na wachezaji wakubwa kama huyo ni faida kwake hasa ikitokea ana mweka benchi hawezi kuchukia wala kufikiria kuondoka.
Alisema changamoto kama hizo ni za kawaida kwenye soka hata akiondoka Yanga atakapokwenda jambo kama hilo linaweza kumtokea hivyo ni bora akabaki na kupambania nafasi yake