Baada ya ushindi wa kibabe wa mabao 3-2 dhidi ya Mwadui Fc, Yanga inahamishia nguvu zake kwenye michuano ya kombe la FA ambapo Ijumaa ya wiki hii, Juni 25 watashuka uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kuikabili Biashara United
Ni mchezo wa nusu fainali ambao wakazi wa Tabora wataushuhudia mbashara baada ya kukosa burudani ya soka la viwango kwa muda mrefu
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanakwenda Tabora wakiwa na lengo moja tu, kushinda mchezo ili kuingia fainali
Aidha, mshambuliaji Waziri Junior aliyefunga bao la ushindi mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, amesema wana kiu ya kushinda mchezo huo
"Haya ni mashindano ambayo sisi tunayataka sana. Tunaona tuna nafasi nzuri ya kushinda kombe hili. Mimi binafsi nahitaji kuvaa medali ya ubingwa, hivyo tutapambana kuhakikisha tunashinda mchezo wa nusu fainali, " alisema Waziri
Mchezo wa pili wa nusu fainali kati ya Azam Fc dhidi ya Simba utapigwa Jumamosi, Juni 26, Songea