Yacouba Songne na Waziri Junior leo wamewakumnbusha Wananchi heshima ya Yanga dhidi ya hizi timu 'ndogo' wakifunga mabao mawili kwenye dakika za nyongeza na kuisaidia Yanga kuondoka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mwadui Fc
Pamoja na kutawala mchezo kwa muda mwingi, kukosekana kwa utulivu kulipelekea Yanga ikakosa mabao mengi ikiwemo nafasi ya mkwaju wa penati aliyokosa Fiston Abdulrazak
Aidha makosa ya mlinda lango Farouk Shikhalo nusura yaigharimu Yanga alama tatu kwa mara nyingine akifungwa bao la umbali wa mita 40
Shikhalo amekuwa na kawaida ya kusogea sana mbele nje ya eneo lake awapo golini, inapopigwa mipira mirefu anafungwa kirahisi sana
Hata hivyo, Wachezaji wanastahili pongezi kwani hawakukata tamaa hata dakika 90 zilipokamilika
Ushindi wa dakika za majeruhi unaifanya Yanga iendelee kushikilia sherehe za ubingwa ambazo watani Simba wanaonekana walikuwa wameanza kuziandaa!
Β