Kikosi cha Yanga leo kinarejea uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc utakapigwa kuanzia saa moja usiku
Ni siku nyingine ya 'shoo shoo' za kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye kwa sasa ndio habari ya mjini
Aidha ni mchezo ambao unaiona Yanga ikiondoka na ushindi mnono kama wachezaji wake watakuwa na utulivu
Mwadui Fc hawana cha kupoteza kwani tayari wameteremka daraja, lakini wanaweza kuwapa changamoto Yanga
Yanga imeshinda michezo miwili iliyopita dhidi ya Mwadui kwenye ligi na robo fainali ya kombe la FA, Wananchi wakifunga mabao saba katika michezo hiyo
Safu ya ushambuliaji ya Yanga leo huenda ikaongozwa na Yacouba Songne aliyekosekana mchezo dhidi ya Ruvu Shooting
Saido Ntibazonkiza, Tuisila Kisinda wanaweza kuanza , kuongeza kasi ya mashambulizi ya Yanga
Yanga bado iko kwenye mbio za ubingwa, ushindi ni matokeo pekee ambayo yataendelea kufanya mbio hizo zisifike kikomo mapema
Ni saa moja usiku pale uwanja wa Benjamin Mkapa