Lamine aomba kuondoka Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jun 2021
Lamine aomba kuondoka Yanga

Imeelezwa nahodha wa Yanga Lamine Moro ameomba kuachwa katika kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria kuelekea msimu ujao

Lamine amepoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza tangu ujio wa beki Dickson Job aliyesajiliwa dirisha dogo akitokea klabu ya Mtibwa Sugar

Majeruhi ya mara kwa mara na tuhuma za utovu wa nidhamu zinatajwa kuwa sababu zinazomfanya asionekane kikosini mara kwa mara

Miongoni mwa nafasi ambazo Kocha Nasreddine Nabi amependekeza kuimarishwa ni safu ya ulinzi, akihitaji beki mwingine wa kati

Lamine bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Yanga lakini kukosa nafasi kunatajwa kuwa sababu ya kuomba aachwe

Hii itakuwa mara ya pili Lamine anaomba kuondoka kabla ya mkataba wake kumalizika

Msimu uliopita alivunja mkataba wake ghafla baada ya kuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara

GSM walipoingia walimrejesha nchini kwa kumlipa madai yote na kumuongezea mkataba mwingine wa miaka miwili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’