Yanga itaendelea kumuenzi hayati Kenneth Kaunda Rais wa kwanza wa Zambia aliyefariki dunia juzi akiwa na umri wa miaka 97
Kaunda alikuwa mdau wa michezo, jina lake litaendelea kubaki katika historia ya Yanga
Uwanja wa Kaunda uliopewa jina lake, alitoa msaada wa kifedha katika ujenzi wake

Uongozi wa Yanga unaendelea na jitihada za kukarabati uwanja huo ili kuhakikisha unaweza kutumika tena
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema uwanja wa Kaunda utabaki kuwa kumbukumbu ya Mzee Kaunda ambaye pia alishiriki kikamilifu kwenye harakati za kudai uhuru wa nchi za Afrika
"Klabu ya Yanga Sc itaendelea kumkumbuka na kumuenzi Hayati Keneth Kaunda kwa kuhakikisha Uwanja wa Kaunda uliopo Makao Makuu ya Klabu, Jangwani unaendelezwa ikiwa ni sehemu muhimu ya kumbukumbu yake katika Historia ya Klabu yetu"