Elimu ya Mabadiliko Yanga inaendelea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jun 2021
Elimu ya Mabadiliko Yanga inaendelea

Mambo mengine matano muhimu unayopashwa kuyafahamu kuhusu mabadiliko ya Yanga

1. Mtaji wa kampuni:

Kwa mujibu wa sheria za makampuni, kampuni lazima itaje mtaji wake kabla haijasajiliwa.

Yanga itathaminisha nembo, chapa yake (trademark & brand) Wanachama na Mashabiki wake, thamani ya hivi vitu vyote ndio utakuwa mchango wake kwenye mtaji wa kampuni itakayoanzishwa.

Thamani halisi ikishapatikana kwa fedha tasilim, 49% ya fedha hizo ndio utakuwa mchango wa wawekezaji.

Yanga itatenga 49% ya hisa zake (approved share capital) kwa ajili ya kuziuza kwa wawekezaji kwa masharti yatakayowekwa na klabu.

2. Nani anaweza kununua hisa:

Kwa watanzania, ni mwanacha chama yoyote na mtu mwenye itikadi za Yanga, Kwa muwekezaji ambaye sio Mtanzania, atauziwa hisa kwa masharti yatakayowekwa kama atakuwa tayari kuyaafata. (Masharti haya yatawekwa wazi siku nyingine).

3. Gawio:

Kama nilivyoelezwa kwenye bandiko lililopita, kwamba Klabu ya Yanga itabaki pamoja na mali yake, isipokuwa majukumu ya uendeshaji wa shughuli za kimpira yatachukuliwa na Kampuni itakayoanzishwa, hivyo basi kampuni hii ikitengeneza faida, Yanga itapata 51% ya gawio na wawekezaji watachukua 49% kwa ujumla wake.

Wanachama wa Yanga kupitia mkutano mkuu ndio wataamua matumizi ya hela hizo zikafanya nini, yenyewe itakuwa inapokea faida tu.

4. Mali za Klabu:

Mali za sasa za Klabu zitaendelea kuwa chini ya Klabu, hakuna mali itakayohamia kwenye kampuni. Kitu pekee kitakachohamia kwenye Kampuni ni uendeshaji wa timu tu.

Kampuni kwenye kukua itatengeneza mali zake (assets) ambazo umiliki wake Yanga itamiliki kwa 51% tu.

5. Kufilisika:

Ikitokea kampuni iliyoanzishwa inafilisika, mali za Yanga hazitaguswa kabisa, ufilisi utaishia kwenye mali za kampuni ambazo zitakuwa zimepatikana katika kukua kwake.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’