Wakati Yanga U20 wakitinga fainali ya ligi kuu ya Vijana kwa ushindi wa mikwaju ya penati 6-5 dhidi ya Azam Fc baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 hapo jana, watani zao Simba walikumbana na kipigo mbele ya Mtibwa Sugar wakiraruliwa mabao 3-1
Mchezo wa fainali sasa utazikutanisha Yanga na Mtibwa Sugar ukitarajiwa kupigwa kesho Jumamosi, uwanja wa Azam Complex
Wananchi walikuwa wakiwatamani watani zao zaidi kukutana nao fainali, lakini sasa wamepanga kuwalipia kisasi dhidi ya Mtibwa Sugar
Mtibwa Sugar ndio mabingwa watetezi wa ligi ya vijana, wanakutana na Yanga inayolihitaji taji hilo msimu huu
Uongozi wa Yanga umeipongeza timu ya vijana wa U20 kwa kufanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo
ADVERTISE HERE