Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting Charles Boniface Mkwasa amekiri kuwa timu yake ilikuwa na wakati mgumu kukabiliana na Yanga hasa kwenye kipindi cha kwanza kutokana na mbinu alizotumia kocha Nasreddine Nabi
Mkwasa amesema vijana wake walikuwa na wakati mgumu kwendana na kasi waliyokuwa nayo Yanga hasa wanapokwenda kushambulia
"Hii Yanga ya sasa ni tofauti na ile tuliyocheza nayo mwanzo. Kuna wakati walikuwa wakitupa hofu kutokana na kasi waiyokuwa nayo wanapokwenda kushambulia kutokea nyuma"
"Hata hivyo kwenye kipindi cha pili tulifanya maboresho ya kimbinu ambayo yalituimarisha. Mpira ni mchezo wa makosa, tulifanya makosa kwenye kipindi cha kwanza tukaruhusu mabao mawili rahisi. Nasi tuliweza kufunga mabao mawili kwenye kipindi cha pili kama sio mpira wa adhabu wa Saido tungeweza kutoka 2-2 au hata kushinda kwani zipo nafasi ambazo nasi tulipoteza," alisema Mkwasa
Nabi amekiimarisha kikosi chake ambapo sasa wachezaji wanaweka mpira chini huku wakionyesha utulivu mkubwa katika kuanzisha mashambulizi
Wana kasi nzuri pale wanapofika kwenye maeneo hatarishi kusaka bao
Mkufunzi huyo wa Yanga mwenyewe anasema vijana wake mpaka sasa wamemuelewa kwa asilimia 40 tu, lakini anaona mwanga, taratibu wanaelekea kule ambako kila mmoja anataka wafike