Nabi afunguka mapendekezo yake kwenye usajili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jun 2021
Nabi afunguka mapendekezo yake kwenye usajili

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amekanusha tetesi zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amependekeza wachezaji 10 wasajiliwe msimu huu

Akizungumza na wanahabari jana baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao Yanga walishinda mabao 3-2, Nabi alisema alitoa mwongozo wa wachezaji aliokuwa akiwahitaji

Kiungo Saido Ntibazonkiza ndiye aliyekuwa mkalimani wa Nabi aliyekuwa akizungumza lugha ya Kifaransa

"Mwalimu anasema hajapendekeza usajili wa wachezaji 10. Alichosema ni kuwa amewaelekeza viongozi maeneo ambayo wanapaswa kuyaimarisha, hakuna idadi ya wachezaji aliowataja"

"Lakini pia bado mpaka sasa hakuna mchezaji aliyeachwa, hajazungumza na mchezaji yeyote kuhusu hatma yake," alisema Saido

Aidha akizungumzia ushindi dhidi ya Ruvu Shooting, Nabi aliwapongeza wachezaji wake kwa kuweza kushinda mchezo huo licha ya kuwa hawakucheza kwa kiwango kile alichotaka

"Wachezaji wangu wamejitahidi ingawa walifuata maelekezo kwa wastani wa asilimia 40 tu. Tumepata wiki mbili za kujiandaa, baadhi ya wachezaji walikuwa na majukumu ya timu za Taifa na wengine majeruhi. Tutaendelee kujiimarisha naamini baadae wataelewa vyema mfumo tunaotaka wacheze. Kwa sasa tutaendelea kupambana kusaka matokeo katika kila mchezo"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’